Ijumaa Novemba 25, Fidel Castro, kiongozi wa Mapinduzi ya Cuba alifariki dunia. Kifo chake kilitangazwa na kaka yake Raul kupitia television.
Amiri jeshi mkuu wa Mapinduzi ya Cuba alifariki saa 22:29 kwa saa za Cuba,” alisema kaka wa Fidel wakati akitangaza kifo cha mdogo wake.
Cuba imetangaza siku za maombolezo hadi Disemba 4, siku ambayo Castro atazikwa kwenye jiji la Santiago.
“Hii yote inaweza ikachukuliwa poa na ulimwengu wa soka lakini kiongozi huyu mashuhuri aliuangusha utawala wa kibabe na kuanzisha ujamaa mwaka 1959 akiwa pamoja na Che Guevara, alikuwa ni msaada mkubwa kwenye maisha ya Diego Maradona,” anasema fundi huyo wa mpira.
Mara ya kwanza Maradona kutembelea Cuba ilikuwa ni mwaka 1986 baada ya kuisaidia nchi yake kutwaa Kombe la Dunia.
Maradona alikutana na Castro na alishangazwa na story zake, baada ya hapo alikuwa akirejea mara kwa mara kwenye visiwa vya Caribbean. Alikuwa akipeleka jezi za soka kama zawadi kwa rais huyo.
Na hapo ndio ukawa mwanzo wa Maradona kupata nafuu huku watu waliokuwa karibu na mchezaji huyo wakati huo wakithibitisha namna Castro alivyookoa maisha yake.
Maradona ametuma salam zake za rambirambi akiwa nchini Croatia ambako alikuwa anaangalia fainali ya Davis Cup: “Alikuwa kama baba kwangu. Fainali hizi zikimalizika nitakwenda Cuba kumuaga rafikiangu. Alifungua milango ya Cuba kwa ajili yangu wakati Argentina walipoifunga.”
Familia ya soka duniani ni lazima imshukuru Castro, shabiki wa baseball,
kwa ajili ya kumuokoa mchezaji wa muda wote. Diego bila shaka atakuwa
aki-enjoy cigar kwa heshima ya Castro.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT