Musoma. Zaidi ya walemavu wa kusikia 50 kutoka Halmashauri ya Mji
wa Musoma mkoani Mara wamepewa mafunzo ya utambuzi wa noti bandia na
halisi ili kuwaepusha kudhulumiwa haki zao.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya utambuzi huo yaliyofadhiliwa na Benki Kuu Tanzania (BoT), Mkurugenzi Mtendaji wa Kikundi cha Sanaa na Utamaduni cha Viziwi Tanzania (Kisuvita), Abibu Mrope alisema walemavu hao wamekuwa wakidhulumiwa haki zao kutokana na kushindwa kubaini noti hizo.
Alisema walemavu wa aina hiyo wengi hawana elimu kutokana na wazazi wao kutowapeleka shule, hivyo hujiajiri katika biashara ndogondogo ambazo ni rahisi watu kuwaibia.
“Uelewa mdogo juu ya noti hizo umesababisha wengi wao kutoendelea kimaisha hata kibiashara kutokana na kupokea fedha nyingi zisizo halali,” alisema Mrope
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT