Askari 6 wa usalama barabarani wafutwa kazi | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Alhamisi, 24 Novemba 2016

Askari 6 wa usalama barabarani wafutwa kazi

Mkuu wa Operesheni, Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Fortunatus Musilimu, amewaondoa ndani ya kikosi hicho askari sita kwa kukiuka maadili ya jeshi la polisi katika utendaji kazi

Askari hao ni kutoka mikoa ya Mwanza, Ruvuma, Mbeya na Tabora na sasa watapangiwa majukumu mengine.

Musilimu ametangaza uamuzi wa kuwaondoa askari hao sita ndani ya kikosi cha usalama barabarani, baada ya kuendesha zoezi la ukaguzi wa utendaji kazi wa askari wa usalama barabani kwenye mikoa hiyo na kuwabaini kufanya vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Aidha  mkuu huyo wa operesheni za kikosi cha usalama barabani amewataja askari hao kuwa ni Sajenti Richard aliyekutwa eneo la Misungwi, PC Edward na PC Mungwe wa mkoani Ruvuma, WP Coplo Mariam wa Igurusi mkoani Mbeya, Staff Sajenti Samwel na PC Dickson wa Igunga mkoa  wa Tabora.

Akizungumzia udhibiti wa madereva wanaofanya makosa ya barabani, amesema kuanzia sasa kuna operesheni itakayofanyika kwenye barabara zote kuu nchi nzima na kwamba madereva wa magari na pikipiki watakaokamatwa wakifanya makosa ya makusudi hawatapewa nafasi ya kulipa faini na badala yake watachukuliwa hatua nyingine za kisheria.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT