Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Sihaba Nkinga, ameitaka jamii ikiwemo wazazi kutambua umuhimu wa
kuwapa elimu watoto wa kike ambao wengi wao wanaikosa kwa kuolewa
wakiwa na umri mdogo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sihaba Nkinga.
Akizungumza katika kongamano la watoto la kuadhimisha siku ya kimataifa
ya mtoto wa kike lililofanyika katika shule ya Mwendakulima wilayani
Kahama, Nkinga amesema vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vimekithiri
ambavyo hivi sasa mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa matukio hayo.
Nkinga amesema kwa mkoa huo wa Shinyanga unaongoza kwa asilimia 59 ya
watoto wa kike kuolewa na kupewa mimba wakiwa chini ya umri wa miaka 18
hali inayowafanya kukosa haki zao za msingi ikiwemo elimu.
Kilele cha siku ya mtoto wa kike kitaifa kitafanyika leo Mkoani
Shinyanga ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia , Wazee na watoto,ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Mimba na ndoa za utotoni zinaepukika chukua hatua kumlinda mtoto wa
kike.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT