Jina la nahodha wa timu ya taifa ya
England na klabu ya Man United Wayne Rooney linazidi kukaa kwenye
headines kila kukicha, Rooney amerudi kwenye headlines kwa mara nyingine
tena baada ya mke wake Coleen Rooney kuoneshwa hisia zake za
kusikitishwa kuzomewa mmewe katika mchezo dhidi ya Malta.
Rooney kwa sasa anaonekana kukutana na
wakati mgumu katika soka lake baada ya kuonekana na kuanza kukosa nafasi
ya kuanza kikosi cha kwanza chini ya kocha Jose Mourinho kwa mechi 3
zilizopita, kitendo cha kuzomewa kwa nahodha siku ya Jumamosi katika
mchezo dhidi Malta Wembley hakikumfurahisha mkewe Coleen Rooney.
“Mechi
kama ya kesho na una mtoto wa kiume ana miaka sita halafu awepo
uwanjani anaangalia baba yake akizomewa, hilo sio sawa kiukweli” tweet hiyo imekuja leo ikiwa yameanza maneno ya kuwa Rooney atakosekana katika mchezo wa kesho dhidi ya Slovenia.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT