1. Asali yenye mdalasini
Chukua asali vijiko vidogo vitatu na uchanganye na mdalasini ya Unga kijiko kikubwa kimoja. Pakaa mchanganyiko huu kidogo kidogo juu ya jino linalouma kutwa mara 3
2. Aloe vera (mshubiri)
Pata aloe vera fresh na uchane kupata maji maji yake (utomvu) na unyunyize juu ya hilo jino linalouma kidogo kidogo kutwa mara 2
3. Mafuta ya nazi na karafuu
Chukua karafuu 3 zitwangwe kwenye kinu, changanya na mafuta ya asili ya nazi kijiko kidogo kimoja uliyotengeneza mwenyewe nyumbani. Pasha kwenye moto kama dakika tatu, ipua na usubiri mchanganyiko wako upoe. Paka mchanganyiko huu juu ya jino linalouma na uache kwa dakika 7 kisha jisukutue kinywa na maji.
Epuka vyakula vitamu sana vya madukani, ice cream, pipi, na soda zote na vingine vya jamii hiyo
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

0 comments:
POST A COMMENT