Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya kati kimeitaka
serikali kuwalipa fidia wakazi wa Manispaa ya Dodoma ambao kwa namna
moja au nyingine wameathirika wakati Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu
(CDA) ilipokuwa ikifanya kazi kwa kuporwa ardhi yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa
Chadema, Benson Kigaila wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake mjini hapa.
Kigaila amesema kuwa Rais John Magufuli hawezi kuivunja CDA na ikawa
ndiyo mwisho wake bila kuangalia madhara yaliyosababishwa na mamlaka
hiyo kwa wananchi katika kipindi chote cha miaka 44 iliyofanya kazi.
Amesema fidia hiyo ni lazima ilipwe na serikali kuu ambayo ndiyo
iliyoiweka CDA madarakani na siyo kuliachia jukumu hilo Manispaa ya
Dodoma kwa kuwa haihusiki na unyang’anyi huo.
"Kuivunja CDA siyo hoja. Hoja inayokuja hapo ni je wananchi wa Dodoma
walionyang'anywa ardhi yao na CDA bila kulipwa fidia watafidiwaje au
ndiyo wataachwa waendelee na maumivu yao?" amesema Kigaila
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT