Moja kati ya habari zinazogonga vichwa vya habari barani Ulaya leo
November 24 ni kuhusiana staa wa kimataifa wa Cameroon anayeichezea
Antalyaspor ya Uturuki Samuel Eto’o kuandikwa kuwa anaweza kukumbana na
kifungo cha miaka 10 jela pamoja na faini.
Stori kutoka 101greatgoals.com imeandika kuwa staa huyo wa Cameroon
anaweza kufungwa miaka 10 jela na faini ya euro milioni 14 ambazo ni
zaidi ya Tsh bilioni 30 kwa kosa la ukwepaji kodi akiwa Hispania katika
kipindi kati ya mwaka 2006 na 2009 kupitia mauzo ya haki ya picha zake.
Eto’o alicheza na kuishi Hispania akiwa anaichezea FC Barcelona kuanzia
mwaka 2004 hadi mwaka 2009 alipoamua kuhama na kujiunga na Inter Milan
ya Italia na baadae kwenda kucheza soka Urusi katika klabu ya Anzhi
Makhachkala.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT