Askari wakiwa nje ya geti la kuingia Stella Maris (Stemmuco) ambako
mkutano wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ulitarajiwa
kufanyika
Mkutano huo ulitegemewa kuanza saa 5 asubuhi lakini askari walionekana wakizunguka geti la kuingia chuo cha Stella Maris (Stemmuco) ambako CUF walitegemea kutumia ukumbi wao.
Katika eneo la chuo hicho yalionekana magari matatu ya askari ambayo pia yalikuwa yakizunguka katika mji wa Mtwara na gari moja la maji ya kuwasha likiwa limesimama kando ya eneo la chuo hicho.
Mkurugenzi wa habari, uenezi na uhusiano wa Umma CUF, Mbarala Maharagande amesema mkutano huo ulilenga kukagua shughuli za chama, kupata maoni ya wanachama pamoja na mapendekezo ya namna ya kuboresha utendaji wa chama kwa ngazi za chini.
Mwandishi wetu aliyeko Mtwara amesema Kamanda wa polisi mkoani humo atazungumza baadaye kuhusu kilichotokea.
Source: Mwananchi
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT