Cuba inaadhimisha siku tisa za maombolezo kufuatia kufariki kwa Fidel
Castro, anayejulikana kwa siasa zake za kimapinduzi, aliyetawala taifa
hilo kwa miongo kadhaa na ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 90.
Mwili wake, utachomwa hadi kuwa majivu kama alivyotaka, katika sherehe
ya kibinafsi, ambapo majivu yake yatazungushwa katika msafara maalumu
kote nchini kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mji wa Santiago Desemba
tarehe nne.
Akiwa kiongozi mwenye mrengo wa kushoto na mwanamapinduzi msifiwa, alipendwa na kuchukiwa na watu mbalimbali kote duniani.
Watu wengi katika mji mkuu wa Havana walidondokwa na machozi kwa kuwa
kiongozi shujaa aliyeweza kukabiliana na Marekani katika uwanja wa
kidiplomasia kwa miongo kadhaa, licha ya mbinu nyingi zilizofanywa za
kutaka kumuua.
Waasi wa Serikali ya Castro hata hivyo walisherehekea kote duniani, walikotorokea.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT