Unaweza kusema siku ya kufanya nyani, miti yote huteleza na ndicho
kilichowatokea KRC Genk anayochezea Mtanzania, Mbwana Samatta.
Samatta ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea TP Mazembe wakiwa mabingwa wa Afrika, alicheza kwa dakika 90.
Genk imepoteza mchezo wake wa Ligi Kuu ya Ubelgiji kwa kuchapwa mabao 6-0 dhidi ya Oostende.
Mechi hiyo ilionekana ya upande mmoja na hasa kipindi cha pili ambacho
wenyeji walipata mabao yao manne baada ya kungoza 2-0 hadi mapumziko.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT