Waziri Mkuu ampa siku 7 Waziri Mwakyembe | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Ijumaa, 25 Novemba 2016

Waziri Mkuu ampa siku 7 Waziri Mwakyembe



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa 21 wa Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe kumpa maelezo kuhusu sababu za Tanzania kutokukamilisha mkataba wa Mawakili wa Afrika Mashariki kutambuana katika utendaji wao.
Waziri wa Sheria na Katiba - Dkt Harrison Mwakyembe
Ametoa agizo hilo leo wakati akimuwakilisha Rais Dk. John Magufuli katika ufunguzi wa mkutano wa 21 wa mwaka wa Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
“Nimeshtushwa kidogo kusikia kwenye taarifa yenu kuwa mkataba huo uliolenga nchi zote za Afrika Mashariki hautaihusisha Tanzania kutokana na kutokukamilisha sehemu yao ya kuufanyia kazi, nitahitaji maelezo,”
“Nitapenda kupata maoni yako wewe mwenyewe Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania kwa vile wewe ni Mwanasheria mwandamizi na siyo Mwanasheria  wa Tanganyika Law Society peke yake kwa nini Tanzania haijakamilisha mkataba huu,” amesisitiza.
Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa maelezo ya awali aliyopewa kuhusu mkataba huo, utakuwa na umuhimu mkubwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kama ilivyo kwenye sekta nyingine zinazoshirikiana ikiwemo uhandisi, uhasibu, uthamini na uchoraji wa majengo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT